Chemical Ataja Vigezo Anavyotaka Kwa Mwanaume
Msanii wa Bongo fleva Claudia Lubalo maarufu kama Chemical amefunguka na kutaja vigezo anavyoangalia kwa mwanaume ambaye anataka kuwa naye.
Chemical amefunguka na kuweka wazi kuwa anapendelea kuwa na Mahusiano na wanaume tofauti na tetesi ambazo zimekuwepo juu ya jinsia yake kutokana na kuoenda kuvaa kiume.
Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Chemical ametaja vigezo ambavyo anaviangalia kwa mwanaume kabla ya kuwa Kwenye Mahusiano naye:
Sitaki mwanaume mfupi maana akiwa kashakua mfupi hatweza kunikiss na wala sitaki mwanaume mnene wala mwembamba awe wa kawaida tu na wala asiwe anabeba vyuma”.
Lakini pia Chemical amesema anapenda mwanaume ambaye atamkubali yeye kama yeye na jinsi alivyo hataki mwanaume ambaye atataka abadili maisha yake kwa ajili yake.