Mwanangu Akitaka Kuwa Mwanamuziki Ruksaa-Madee Ali
Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Tip Top Connection, Madee Ali amefunguka na kudai endapo binti yake atakuwa na ndoto ya kuwa msanii hawezi kukataa.
Madee Ali amesema atamruhusu binti yake huyo anayeitwa Aimal Hamad kuwa msanii kwa sababu yeye alivyokuwa mdogo alifuata nyayo za Baba yake na kuingia kwenye sanaa.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo5 hivi karibuni Madee alisema licha ya mara nyingi kuwa na wanae hata studio hajui iwapo atapenda muziki lakini yeye kama mzazi hawezi kumuwekea mipaka.
Tunashauriwa tuwaangalie watoto wafanye kile ambacho wanapenda kwa sababu anaweza kuwa anapenda mpira mimi nikamzuia nikamwambia afanye kitu kingine na asifanikiwe, nitakuwa nimepata lawama.
So akielekea huko mimi sina tatizo kwa sababu hata mimi mwenyewe nimemfuata baba yangu alikuwa ni mwanamuziki wa Western Tabora Jahazi Band wala hakutegemea nitakuwa mwanamuziki, so sitaona maajabu sana kwa sababu Waswahili wanasema maji hufuata mkondo”.
Kuna wasanii wengine wengi ambao wana maoni tofauti ambao wanaweza wazi kuwa hawataki watoto wao wake kuingia kwenye sanaa hapo baadae.