Ali Kiba Amedai Kuwa Hata Kama Ni Staa Hawezi Kuishi Maisha Ya Kujionyesha
Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kudai kuwa pamoja na kuwa na umaarufu mkubwa lakini hataweza kuishi maisha ya kujionyesha mbele za watu.
Lakini pia Ali Kiba ameonekana kuwatupia Dongo wasanii wenzake wanaoishi maisha ya kujionyesha (show off) na kudai kuwa kuna maisha ya kuishi kama staa Lakini pia kuna maisha ya kuigiza kuwa staa.
Ali Kiba amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Dj Show ya Radio One ambapo amedai maisha anayoishi ndio yana manufaa sana kwa mashabiki zake ambao walimuwezesha kufika hapo.
Kuna maisha ya ustaa na kuna maisha ya kawaida na kuna maisha ya kuigiza kuwa staa. Mimi sijachagua in nature nipo hivyo, Watanzania walinipokea katika hali ambayo kiukweli haisemeki sasa hii leo nije nibadilike, so nisingependa kumshawishi shabiki yangu kwa namna yoyote ile kuwa nimebadilika kwa sasa hivi.
Kwa hiyo ule wivu wa kumfanya mtu anze kunichukia kwamba Ali amekuwa hivi na hivi, hapana!. Mimi ni staa, mimi ni supa staa nitafanya, ninaishi maisha ambayo nimechagua lakini bado nitaendea ku-humble kwa watu“.
Ali Kiba ameendelea na media tour kwa ajili ya kutangaza Single yake mpya ya ‘Mvumo wa radi’ ambayo imeendelea kushikilia namba moja Kwenye mtandao wa Youtube.