Davina- Baada Ya Kuachika Sana Kwenye Ndoa Nimejifunza Mengi
Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Halima Yahaya amefunguka na kudai kuwa pamoja na kwamba ameachiwa sana kwenye ndoa zote alizowahi Kuolewa lakini amejifunza mambo mengi kupitia huko.
Davina amekiri kuwa ni kweli hajawahi kupata bahati ya kukaa na mume kwa muda mrefu lakini amejifunza kuwa mwanamke jasiri na shupa I na kuweza kujua kuwa kujituma na kuweza kuwalea watoto wake mwenyewe.
Kwenye mahojiano na Amani kwa njia ya simu, Davian alisema Mungu amemjalia kupitia kwenye ndoa mbili lakini hakubahatika kukaa kwa muda mrefu lakini kikubwa ni kwamba ndoa hizo zimemfunza mambo mengi sana ya kujituma ili aweze kuwalea watoto wake vizuri.
Siwezi kujilaumu hata siku moja kwa nini sikai kwenye ndoa zote nilizozipitia bali ninachojua ni kwamba zimenifundisha mambo mengi sana hasa ya kujisimamia mimi kama mimi na kuendesha familia nikiwa kama mwanamke mwenyewe bila mtu mwingine pembeni”.