Bella Adaiwa Kumtelekeza Mtoto Wake na Kushinda Baa
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Isabella Mpanda maarufu kama ‘Bella’ amekumbwa na skendo ya kumtelekeza mtoto wake ambaye ni kichanga.
Habari za chini ya kapeti zinadai Bella amegoma kumnyonyesha mtoto wake ambaye alimzaa Miezi michache iliyopita na hata kumwacha mtoto huyo nyumbani huku akienda kukaa Kwenye mabaa.
Chanzo kilieleza kwamba, mwanamama huyo amekuwa akishinda siku nzima hadi usiku akitoa huduma baa huku akimwacha mtoto huyo mchanga, hali inayozua maswali kwa watu wake wa karibu kwamba, inakuwaje anamwacha, si anaweza kukosa malezi bora maana maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga hadi miezi sita?
Baada ya tetesi hizo, Za Motomoto News ilimtafuta Bella ambaye alikiri kuwa kweli, baada ya kujifungua alikaa siku chache tu ndani kabla ya kuanza kazi ya kuhudumia kwenye baa yake ila amekuwa akienda kumnyonyesha mwanaye kila wakati.
Unajua watu wanashindwa kuelewa, baa iko hapa karibu na ninapoishi, kwa hiyo natoka asubuhi kuja kusimamia na kuuza chakula na jioni pombe, nimekuwa nikirudi nyumbani mara kwa mara kumnyonyesha mtoto kwa kuwa sitaki kujilegeza na napenda kutafuta pesa na wateja wanahitaji kuniona ninawahudumia mimi”.