‘Agness Aliishia Form Two, Alinipigia simu akaniambia byee”, Baba wa Marehemu Aongea

Baba mzazi wa marehemu Agness Masogange amefunguka makubwa na mazito ambayo inawezekana watu wengi walikuwa hawayajui kuhsu agness masogange hata kama walikuwa wakimfahamu kama rafiki au mfanya kazi mwenzao.

Mzee Gerald Waya maefunguka na kusema kuwa pamoja na yote lakini agness kwake alikuwa ndio nguzo kubwa aliyekuwa akiitegemea sana katikamaisha yake na msiba huo umekuwa pigo kubwa sana kwake.

download latest music    

Mzee Gerald ansema kuwa agness alikuwa mtoto wa nne kati ya watoto sita huku watano wakiwa wa kike na alisoma shule ya msingi Utengule mkoani Mbeya wilaya ya Mbalizi ambapo alipofika form two ,Agnesss alishindwa kuendelea na masomo yake kutokana na matatizo aliyoyapata.

Aliishia form two, akapata matatizo, tukakosana kidogo lakini aliamua kwenda dar lakini tuliwekana sana kabla ya kuondoka., mwanangu alikuwa nguzo kwangu, alikarabati nyumba hii ninayoishi na alikuwa msaada sana kwangu niliposikia msiba huu niliumia sana.

Niliongea nae kabla ya kifo chake akaniambia anaumwa, nikamuuliza ni nini akasema tu wewe niombee kwa mungu, jumamosi iliyofuata nikampigia kumuuliza maendeleo yake, hakuniambia kitu akasema byee baba, akaanza kulia na kukata simu.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.