Mama Mkwe wa Alikiba afunguka kuhusu ndoa ya Alikiba na umri wa mwanae
Mama mkwe wa msanii Alikiba ambae ni mama wa mke wa halali wa mwanamke aliefunga ndoa leohuku mjini mombasa ameonekana kufurahia jambo hilo huku akisema kuwa kwao ni kheri kwa mtoto wao kufunga ndoa na ni jambo ambalo hawakuwahi kulijua kama lingeweza kutokea lakini mipango ya mwenyezi mungu ndio ilishatimia.
Akiongea na waandishi wa habari mama wa Amina Rakesh amesema harusi hiyo inategemewa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 400 katika ukumbi wa Diamond Jubilee huko Mombasa.
” kama familia jambo likisha pangwa na mwenyezi Mungu huwezi kuliondosha,hiyo ni siri yake sababu kijana ametoka tanzania amekuja huku kenya, mimi sikujua kama mwanang ataolewa na alikiba lakini mungu ndio aliopanga.Mtoto wangu ana miaka 23 na ni mtoto wangu wa mwisho.