Monalisa Kuikabidhi Tuzo ya APA Bungeni
mwanadada Monalisa amabe ametua bongo siku ya jana kutokea nchin Ghana alipokwenda kwa ajili ya utaoji wa tuzo za african prestigious ambapo yeye pia ni mmoja kati ya walioshinda tuzo hizo kwa upande wa wanawake na Ray Kigosi kwa upand wa wanaume anatarajiwa kuipeleka tuzo hiyo bungeni siku za hii karibuni ikiwa ni kama nembo ya ushindi wa taifa.
Monalisa ambae pia alimpokelea rais wa Tanzania , tuzo hiyo na kuileta nyumbani baada ya Mh Magufuli kuchaguliwa kama kiongozi bora wa Africa, anatarajiwa kwenda bungeni kwa ajili ya kuipeleka tuzo hiyo.
Akiweka bayana hilo , mama wa msanii monalisa anaejulikana kama Mama Natasha amesema kuwa baada ya monalisa kurudi kutoka Accra Ghana anatarajiwa kupokelewa jijini na kisa kwenda Dodoma kwa ajili ya kuipeleka tuzo hiyo Bungeni.
Hata hivyo katika ukurasa wake wa instagram, Monalisa amewshukuru watanzania wote kwa zaidi ya miaka 19 sasa tangu ameanza sanaa mpaka sasa wamekuwa nyuma yake na kusema kuwa hata tuzo aliyoipata ni kwa ajili ya wote na sio peke yake kwa sababu bila mashabiki wake isingewezekana.