Bifu Kati Ya Wanamuziki Ni Muhimu-Country Boy
Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya miondoko ya kurap Ibrahim Mandingo maarufu kama Country Boy ameibuka na kutetea uwepo wa bifu miongoni mwa wasanii.
Bifu ni kitendo cha kutokuwepo maelewano baina ya watu na hii inatumika baina ya wasanii ambapo kwa nchi za nje wasanii hutengeneza bifu ili kuuza kazi zao.
Country Boy amefunguka na kudai bifu ni muhimu katika sanaa na bila kuwepo kwa bifu kunakuwa hakuna msisimko katika kazi za wasanii kwani ushindani unakuwa mdogo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Star Showbiz, Country Boy alisema kuwa, msisimko kwenye muziki unapungua kwa sababu wanamuziki wengi kwa sasa wanaogopa masuala ya bifu bila kufahamu wanalikosesha soko msisimko ambao ungekuwepo kama kunapotokea tofauti.
Unajua muziki ni mashabiki, sasa kunapokuwa na wanamuziki wawili wana tofauti hata mashabiki wao pia wanakuwa wanashindana na kutamba kuonesha kwamba mwanamuziki wao ni mkali kuliko yule mwingine“.
Kwa upande wa muziki wetu wa Bongo fleva moja kati ya bifu maarufu ni kati ya wasanii Diamond Platnumz na Ali Kiba ambao imesemekana kuwa bifu imewasaidia sana kuuza muziki wao.