Uchungu Upo Ila Inabidi Kuacha Kumlilia-Aunty Ezekiel

Staa mkubwa wa filamu za bongo Aunty Ezekiel amesema kuwa hakuna sababu ya kuendelea kumlialia staa mwenzao wa filamu aliekuwa gwiji steven kanumba zaidi ya kumuombea na kufuata nyayo zake ili kukuza kazi za sanaa.

Aunty anasema kuwa uchungu na kumbukumbu yake badio itaendelea kuwepo ila kwa heshima kubwa ya kumuonyesha steven ni kuiga mambo mazuri aliokuwa akifanya ili kuendelea kumuenzi.

download latest music    

Aunty anasema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakilia sana inapofika siku ya kukumbuka siku ya kifo chake,kitu ambacho yeye anaamini kuwa inarudisha tasnia ya filamu nyuma kwa sababu ya kusononeka kwao.

Najua uchungu upo lakini inabidi sasa tuache kulia,badala yake tujitahidi kufika pale ambapo na yeye alitaka tufike na tusonge mbele lakini tukisema kuwa kila siku tubaki tunasononeka hatuwezi kufika tunapopataka hata siku moja.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.