Hanscana Amtetea Darasa, Asema Maneno ya Mashabiki Yanam-panikisha Darasa
Muandaaji wa video bongo Hanscana amefunguka na kumtetea Darasa kwa kuzingatia kuwa yeye ni moja ya watu wa karibu sana na msanii huyo na alikuwa nae kwa kipindi chote ambacho aliweza kufanya nae ngoma za huko nyuma ambazo zilifanya vizuri sana,
Akiongea na Shadee wa Clouds E ,Hanscana anasema kuwa ni kawaida kwa wasanii kukaa kimya kwa muda ili kujipanga na sio Darasa tu ambae amekaa kimya bila kutoa ngoma mpya lakini kwa nini watu wamekuwa wakimkomalia sana Darasa.
Akitolea mfano wa wasanii wengine kama Bob Junior, hanscana ansema kuwa wapo wengi wamekaa kimya lakini hiyo inakuwa ni umauzi wa mtu kujipanaga ili kurudi upya hivyo watu wasihofie swala la Darasa kukaa kimya.
Hanscana anasema kwa jinsia mbayo mashabiki wamekuwa wakiongea katika mitandao ya kijamii kuhusu Darasa , kama msanii huyo asingekuwa jasiri basi angekuwa amesha-panic sana na hata kuamua kuwaridhisha mashabiki kwa kutoa ngoma mpya lakini kwa kukurupuka kitu ambacho baadae wangesema tena ameharibu.
HLlakini pia , hanscana anasema kuwa anachoamini ni kwamba mashabiki wanampenda sana Darasa na ndio maana wamekuwa wakimsumbua yeye sana na wala sio wasanii wengine lakini pia Darasa kwa sasa anapaswa kuwa imara sana ili kuosikiliza maneno ya mashabiki na kujikuta anakurupuka na kutoa ngoma bila kujipanga vizuri.
Maneno ya Hanscana yanakuja baada ya watu wengi kusema kuwa msanii Darasa amekuwa kimya sana na wanahisi kuwa msanii huyo anaweza kuwa na matatzo au ameharibikiwa kabisa na kwamba amefulia hawezi kufanya tena kama mwanzo,hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Hanscana kuongea hayo kuhusu Darasa huku akisema kuwa msanii huo anajipanga ili kutoa kivingine tena.