Harmonize Akiri Kuwa msanii wa Pili Mwenye Nyumba Kali Kuliko Wasanii Wote
Harmonize amefunguka na kuongelea maendeleo anayozidi kuyapata katika muziki huku akisema kuwa katika wasanii wenye nyumba kali bongo yeye atakuwa msanii wa pili endapo nyumba yake itaisha huku nafasi ya kwanza akimuweka bosi wake Diamond.
Harmonize ambae kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa kwangaru aliomshirikisha Diamond platinumz anasema kuwa nyumba yake iko mbioni kuisha na pia hata hiyo ya diamond iko mbioni kusiha na ndio watakuwa wasanii wanaoongoza kuwa na nyumba kali .
Nasema ukweli mimi nyumba yangu ikiisha, nyumba yangu ninayoijenga mimi sijui nitakuwa msanii wa pili Dar Es Salaam kuwa na nyumba kali kuliko wasanii wote bongo wa kwanza ni Diamond ambae pia nyumba yake haijaisha ila ipo katika hatua za mwisho.
Harmonize anakiri kuwa mafanikio makubwa anayoyapata kwa sasa ni kutokana na kufuata ushauri mzuri anaokuwa anapewa na mpenzi wake Sarah.