Diamond Awakosoa Watu Waliodhani Huu Utakuwa Mwaka Wake wa Mwisho Kimafanikio
Staa wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amewazodoa wale wote waliohisi huu utakuwa mwaka wake wa mwisho kimafanikio.
Diamond ambaye umeuonyesha ulimwengu kuwa hakuna kitu kinachomshinda kufanya kuanzia kuwa mmiliki wa record label kubwa Tanzania WCB na hivi sasa mmiliki wa Kituo cha televisheni cha WASAFI TV.
Diamond amesema kuwa jakuna kinachoshindikana kama utaweka juhudi ya kweli na kazi katika kile unachokifanya basi mafanikio ni lazima Diamond ameyadhihirusha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka posti mbili.
Posti ya kwanza Diamond ametoa ahadi jinsi Wasafi Tv itakapotoa usawa kwa wasanii wote bila ubaguzi na kumpa nafasi ya kweli kila mwanasanaa:
Lakini pia katika posti yake ya pili Diamond ameongelea ujasiri alionao na huo ndio unampa mafanikio kwani anapenda kuthubutu kufanya mambo ambayo wengine wanadhani hayawezekani na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kukata tamaa bali ana Songa mbele kutafuta mafanikio.