Christian Bella Atoa Siri ya Kutoboa Kimuziki Bongo.

Msanii wa muziki wa dansi bongo mwenye asili ya kikongo Christain Bella amefunguka na kutoboa siri na tabia ya wakongo na kwanini yeye ameweza kufanya vizuri kimuziki bongo na sio wakongo wenzake huki nchini kwao.

Christian Bella anasema kuwa ukiwa nchini Kongo ni vigumu sana watu wa kule kukuelewa au kuelewa muziki wako kama unatumia lugha nyingine tofauti na ile ya kilingala.Christain Bella anasema kuwa ili uweze kutengeneza mashabiki wa muziki wako ni lazima uweze kufanya muziki kwa lugha wanayoilewa wao.

download latest music    

Kuna ugumu mkubwa wa lugha kwa sababu kule mara nyingi wanapenda sana kilingala,kuna sehemu wanaongea kiswahili na huko ndipo ngoima za bongo  zinakuwa zinahit pia.ugumu ni kwamba wao  ni wabishi sana mpaka wakupitishe na kukukubali na lugha unayoitumia ni wabishi sana.

Hata hivyo Christian ana sema kuwa kutoboa kwake bongo na nje ya nchi ni kwa sababu watanzania wamemuelewa na kuamua kumfanya kuwa msanii wa ndani na nje ya nchi  na ndio maana hata huko kwao ameweza kutangazika sana.

Kwa ugumu wote wa ngoma za kongo na kutumia kwangu kiswahili niliweza kupata  nafasi  kwa  sababu watanania waliweza kunikubali na kunipa nafasi pia, wengi wao walikuwa wanashindwa kujua kama mimi ni mkongo au ni mtanzania. unaweza kuwa unajua sana na bado wakakukataa lakini ukifanya kitu kizuri nje ya nchi ukirudi nchini kongo wanakupokea.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.