Muuaji Wa Marehemu Radio Akiri na Kuomba Radhi

Ni miezi miwili imepita tokea marehemu Radio afariki February 1, 2018, Radio ambae alikuwa pamoja na Weasel wakiunda kundi la Goodlyfe kutokea nchini Uganda, msiba wa Radio uligusa watu wengi duniani.

Baada ya Radio kufariki mtuhumiwa Wamala Godfrey alias Troy anayedaiwa kusababisha kifo cha Radio alikimbia na hakuonekana kwa wiki kadhaa lakini baada ya polisi kuendesha msako wa walifanikiwa kumkamata.

download latest music    

Wamala Godfrey alias Troy amekiri kuwa alisababisha kifo cha Radio na kusema kuwa Radio alimponyoka mikononi mwake na kujipigiza kichwa chake chini wakiwa wanapigana haikuwa lengo lake kumuua na hivyo kuomba msamaha.

Kundi la Good life lilioundwa na Radio and Weasle lilitamba vyema miaka ya nyuma kwa vibao vyao maarufu kama vile bread and butter, Zuena na nakudata.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.