Riyama Ally Amwaga Machozi Baada Ya Kukosa Tuzo Awataka SZIFF Wamuombe Radhi

Muigizaji wa Bongo movie Riyama Ally ameonyesha hisia zake juu ya tuzo za Sinema Zetu International Film Festival zilizofanyika wiki iliyopita baada ya Kukosa tuzo.

Tangu tuzo hizo zifanyike wiki iliyopita zimezidi kuwa gumzo kwani baadhi ya wasanii wa Bongo movie wameonyesha kutokuridhika baada ya kukosa tuzo na wasanii wengine kupata tuzo.

download latest music    

Wasanii kama Batuli na Irene Uwoya wameweka wazi kuwa hawajapendezwa na kitendo cha Wema kushinda tuzo ya msanii bora wa kike na kuamini kuna swankiest wengine wanaofanya vizuri kuliko wao kwenye tasnia hiyo.

Riyama Ally pia ni moja kati ya wasanii wa kike ambaye ameweka wazi kuwa anaamini alistahili kushinda tuzo hiyo na kwenye Interview na XXL ya Clouds FM Riyama Amedondosha machozi huku akiwalaumu SZIFF kwa kumshindanisha kwenye Tuzo ambazo hakuwa hata na taarifa nazo:

Kiukweli hawa watu walioandaa hizo tuzo hawakuniambia chochote na sijui chochote heshima yangu mimi ili wapi? Mimi sijaingia kwenye sanaa ili niweze kutumia fursa niweze kufanya mambo mengine nimeingia kwenye tasnia ili niweze kuelimisha jamii na niweze kupata kipato kwa sababu mimi sijasoma lakini Nina kipaji sana na nimepambana sana Watanzania wanajua Sasa kwanini leo hii watu wanaandaa kitu kinachotaka kunivunjia heshima yangu? 

Mimi sijashindana na mtu yoyote inakuaje nashindanishwa na taarifa sina Mpaka mashabiki zangu hawana habari kusema kweli nimeumia sana na hao was ndani wa hizo tuzo wamenikosea sana Na mimi tamko langu ninalotamka ni Kuwa waandaji wa tuzo hizo waniombe radhi na wawaombe radhi Watanzania kwani wanataka kuniharibia kazi yangu kwani mimi ni Brand Ambassador”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.