Belle 9 Akiri Alishawahi Kufumaniwa.

Msanii wa bongo fleva Belle 9 amefunguka na kuweka wazi kuwa alishawahi kufumaniwa na mpenzi wake akitoka na mwanamke mwingine lakini sababu kubwa anasema kuwa wasanii wengi wa kiumewamekuwa wakitongozwa na wanawake hivyo kuna muda hata wao wanashindwa kujizuia.

Belle 9 ambae alifunga ndoa mwaka jana na mpenzi wake wa muda mrefu na kuamua kufanya siri bila ya watu kujua mpaka pale alipoamua kuweka picha katika mitandao anasema kuwa ni vigumu sana kuepuka maswala ya kufumaniwa kwa sababu wasanii wengi wanakuwa wanatakwa kimapenzi na wanawake.

download latest music    

Nilishawahi kufumaniwa ingawa ni mara chache sana,wanawake wengi huwatamani wanaume wasni kimapenzi, na hii utokea kutokana na ushawishi wa wasanii.lakini mimi nataka mwanamke wangu ajitambue kabisa-Alifunguka Belle 9 alipokuwa akiongea na radio Kings FM.

Vishawishi vinavyotoka kwa wanawake kwenda kwa wasanii vimekuwa b=vingi na wasanii wengi wamekuwa wakikiri kutongozwa na wanawake katika mitandao ya kijamii, hata hivyo kwa sasa Belle 9 ameoa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.