Aliyoyasema Wema Baada ya Kupokea Tuzo
Malikia wa bongo movies, Wema Sepetu juzi aliweza kupokea tuzo kwa kushinda vinyang’anyio mbalimbali huku filamu yake ya heaven sent ikiwa imemsaidia kupata tuzo hizo.
hata hivyo baada ya kupokea tuzo hiyo akiwa palple jukwaani wema alipata nafasi ya kuzungumza juu ya tuzo hiyo ndipo aliposema kuwa kuna baadhi ya kundi la watu wamekuwa wakitaka kumuangusha na kuonekana hafai bongo movies wakati amekuwa akijitahidi kufanya kazi.
Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru alla’h sub’banah wata’Allah kunifikisha hapa nilipo..najua kuna mambo mengi yamefanyika kwa ubaya ila yeye ndio amekuwa tumaini langu kubwa..namshukuru sana mama yangu mzazi na familia yangu kwa ujumla na kusimama na mimi bega kwa bega katika kila kitu
Hata wiki moja haijapita tangu kupokea kwa tuzo hizo, baadhi ya wasanii wa bongo movies wameanza kukwaruzana na kutupiana vijembe kuwa Wema amependelewa na haikuwa haki yake.