Nay wa Mitego Awasilisha Kazi Yake BASATA
Msanii anejulikana kwa shida ya kuwa mbishi na mkorofi inapofikia kwenye swala la kazi zake,nay wa mitego amesalimu mari baada ya kuamua kupeleka kazi yake ya muziki BASATA kukaguliwa kabla ya kutolewa katika vyombo vya habari.Ney ambae pamoja na kwamba amepelaka nyimbo hiyo kwenda kukaguliwa lakini anasema kuwa hiyo haimzui yeye kufanya lolote atakalo katika muziki wake.
Nay wa mitego amesema kuwa kilichomsukuma kupeleka nyimbo yak BASATA ni kukwepa lawama za serikali lakini haimapngii au kubadilisha kile anachokiimba kwa sababu hicho ndicho kinachomwingizia ela na kinampa mashabiki.
Najaribu kufuata utaratibu na nadhani hii ndio ngoma yangu ya kwanza kabisa kuwatumia BASATA , nafanya muziki wangu kama vile nilivyokuwa nafanya , nimepunguza vitu kidogo tu , siwezi kuhama kwenye muziki wangu , yaani nitaendelea kufanya muziki wangu ule ule.Nimewafikishia wimbo wangu sio kwa sababu nataka wanipangie mashairi ya kuimba ila tu sitaki kuanza kuzuiliwa nyimbo zangu.
Maamuzi ya Nay yanakuja baada ya kuwa na wimbo kubwa la wasanii wanofungiwa nyimbo zao kwa sababu ya nyimbozao kukosa maadili katika jamii.