Yawezekana Hii ni Sababu ya Kutumbuliwa kwa Jokate
Habari zilizo chini ya kapeti na ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa kutumbuliwa kwa mrembo jokate katika nafasi yake ya kaimu katibu wa uhamisishaji kwa vijana wa UVCCM kumesababishwa na nafasi hiyo kuatak kupewa msanii mweingine wa kike bongo ambae amehamia CCM hivi karibuni.
Pamoja na kwamba baaada ya kutumbuliwa kwa mwanadada huyo hakutaa kusema kitu chochote kuhusu sababu iliyofanya atolewe katika nafasi hiyo lakini watu mbalimbali wameanza kusema kuwa kutokana na Wema Sepetu kuhamia CCM wa sasa inawezekana nafasi hiyo itakuwa imewekwa wazi ili aweze kupewa yeye baada ya muda.
Akitoa habari hizo moja ya watu wa karibu amesema kuwa inawezekana kabisa kuwa nafasi ya jokate atapewa wema na kisha wema atapewa nafasi kubwa zaidi ingawa kwa sasa jambo hilo limekuwa ni siri kwa sababu ni mambo ya uongozi na muda mwingine inabdi kutunza siri.
Hata kaimu katibu mkuu wa UVCCM, amesema kuwa swala la kuondolewa kwa Jokate ni kitu cha kawadia kabisa kwa kuwa mpaka wanafanya maamuzi hayo ni kwamba walishajiridhisha na maamuzi hayo na sababu za kumtoa zinakuwa zimewaridhishwa wanakamati wote.