BASATA Wakanusha Kufungulia Nyimbo za Diamond.
Siku mbili zilizopita baada ya msanii diamond kukutana na waziri Mwakyembe na Naibu Waziri wake Juliana Shonza ambae alikuwa katika vita ya kurushiana maneno na msanii huyo walipokutana na kuzungumza maswala yaliyokuwa yanaendelea kuhusu kufungia nyimbo za wasanii zikiwemo hizo mbili za Diamond Platinumz kuna baadhi ya mitandao walizusha kuwa nyimbo mbili za Diamond zimefunguliwa na kuruhusiwa kuchezwa kama mwanzo katika vituo vya habari.
katibu mtendaji wa BASATA amesema kuwa habari zinazosambaa wanatakiwa kuzipuuzia kwa sababu hazina ukweli wowote,lakini pia mngerza ameelezea kwanini msanii Diamond amekuta na waziri na wala sio wasanii wengine waliokuwa wamefungiwa.
katibu mtendaji wa BASATA anasema kuwa sababu kubwa ya Diamond kukutana na waziri na Naibu ni baada ya kutokea kwa majibizano kati yao hivyo walitakiwa kukutana hili kuyamaliza matatizo hayo ambayo yalikuwa yanaendelea bila wao kukutana.
Hata hivyo Mngereza maesema kufunguliwa kwa nyimbo ya msanii yoyote ni baada ya msanii huyo kukamilisha vigezo vyote na masharti atakayotakiwa kuyatimiza.