Tunamheshimu Alikiba, Alikiba ni mheshimiwa,:Bahati
Msanii wa muziki wa bongo fleva amabe amekuwa akikubalika sana nchini Rwanda na mashabiki wake sasa hivi ataaanza kufanya kazi nchini humo hivyo kuwa na fursa kubwa ya kuwa karibu na mashabiki zake kwa kipind chote atakachokuwa nchini humo.
Akiongea kwa hamasa moja yya wasanii wakubwa na maarufu nchini humo anaejulikana kama Bahati , amesema kuwa kutokana na ufanyaji kazi mzuri na kujituma kwa alikiba kuna vitu vingi vimewasukuma na kuamua kufanya kazi pamoja na wameangaika sana mpaka kufanikiwa kufanya kazi pamoja lakini wamefanikiwa.
Tulipitia njia nyingi sana kumtafuta Alikiba, kuna kipindi tulikutana ana kwa ana hapa hapa nchini rwanda, tumeungwanishwa na haruna niyonzima maana na alikiba ni marafiki sana na sasa Alikiba ni rafiki yetu.
alikiba ni msanii mkubwa sana na ni msanii ambae namkubali sana, na tuna deal nae kwa sasa,alikiba ni mheshimiwa na tunamheshimu sana , ndani ya dar es salaam kuna wasanii wnengi sana na wote ni mastaa kuna huyou Harmonize, kuna Diamond , rayvanny lakini tumetaka kufanya kazi na Alikiba.
Hivyo basi msanii alikiba na Bahati wanatarajia kuanza kufanya kazi pamoja kwa sababu tayari wasaii hawa walishakaa chini na kukubaliana kufanya kazi pamoja kwa ajili ya mashabiki wao.