Uoga kwako ndio kufeli kwako:Ujumbe wa Aunty Ezekiel kwa Diamond
Mwanadada Aunty Ezekiel arusha kombora kwa waliofungia nyimbo za wasanii !!. Muigizaji huyo wa filamu ameandika haya katika ukurasa wake wa instagram huku akimtaja diamond platinumz kama shujaa katika kusimama imara ili kutetea muziki huo.
.
“Uoga wako ndio kufeli kwako…..diamondplatnumz Am so proud of u kiukweli unajua unachokifanya haijalishi anaetaka kukukatisha Safari yako ni Nani na ana cheo gani ! Ilimradi unajua haki yako basi weka uwoga pembeni na kutetea haki yako….SAFI SANA ….Ktk kazi hizi kwa asilimia kadhaa hawa watu wamekuwa wakichangia kufeli kwa kazi zetu tena Mbaya zaidi hutokeza baada ya kuona kuna baadhi ya mafanikio kupitia fani hiyo Ila wakati mkihangaika kusukuma gurudumu huwa wamekaa kimya kama hawapo. Mnakosea Sana tena Sana mnakatisha tamaa, mnafelisha watu Pamoja na Maisha yao bila kufikiri kuna watu wangapi Nyuma yake ambao anawabeba na kufanya Maisha yaende….Nashindwa kuandika sana lakini natamani tuu wajue kuwa WANATUKOSEA SANA SANA SANA……Wasanii tuinuke na kuwa na Uthubutu wa kusema yote yale ambayo tunaona tunaonewa na sio kukaa kuongea chini chini haitatusaidia na tutaendelea kufeli na wao wakifaulu kwa kuonekana wafanyakazi Bora kumbe hamna lolote Uonevu tuu…
Hata hivyo baada ya mwanadada huyo kuongea hivyo diamond platinumz alimjibu na kusema:
“Ni muda wa kujenga Sanaa iliyo kubwa na yenye kuleta mafanikio kwa wasanii na serikali….sio kuleteana figigufigisu kisa eti una mamlaka kutafuta eti Kiki ama eti uonekane we flani uogopewe HELL NO !