Aliyefungia Wasanii Na Nyimbo Zao sio Mh .Shonza.
Naibu waziri wa habari na michezo Mh Juliana Shonza amefunguka na kusema kuwa aliyefungia nyimbo za wasanii na baadhi ya wasanii kufanya kazi sio yeye kama watu wanavyofikiria ila ni mamalaka inayohusika na swala hilo.
Juliana Shonza ameamua kufunguka hayo siku chache baada ya msanii Diamond Platinumz kwenda katika media na mitandao ya kijamii kulalamika kuhusu kufungiwa kwa nyimbo zake na kufungiwa kwa mwenzo Roma Mkatoliki.
Amewataka wasanii na wananchi kwa ujumla kujua kuwa sio yeye aliyefanya hivyo bali ni mamlaka husika.”Aliyewafungia wasanii sio shonza bali ni mamlaka husika na kama mnavyoona sasa hivi hadi mamlaka ya mawasiliano tanzania , TCRA imeingilia kati swala hilo.sasa mtu anarusa tuhuma kunilaumu anakuwa hanitendei haki kwa kweli”.
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wasanii wakielekeza tuhuma zao kwa naibu waziri Juliana Shonza juu ya kufungiwa kwa wasanii wengi wa muziki kutokana na swala la maadili.