Mimi Sipendi Viben Ten:-khadija kopa
Msanii wa muziki wa taarabu nchini, Khadija Kopa amefunguka na kuongelea swala lake la yeye kutembea na watoto wadogo ambao anawazidi umri na kusema kuwa kwa upande wake hapendi kabisa kutembea na viben ten na hatokaa afanye hivyo hata kama dini inaruhusu.
Khadija Kopa amesema kuwa licha ya kuwa yeye hapendi wanaume wa dizaini hiyo lakini hiyo isiwe sababu ya kuwasema wanawake ambao wamejiingza katika mahusiano na watu hao.
Mbona nyie wazee mnaoa wanawake wadogo na wala sisi hatusemi,sisi kila siku viben ten viben ten weee, mimi sipendi viben tena mimi nilikuwa na mume wangu kabisa na hata katika dini yetu inaruhusu maana mtume alitufungulia njia.
Hata hivyo Khadija Kopa aliweka wazi na kusema kuwa baada ya mume wake kufariki kwa sasa yupo tayari kuolewa na mwanaume yoyote ila awe ameanzia miaka 40 na kwenda juu.