Miss Arusha Amuomba Tunda Kumuacha Baba Watoto Wake.
Siku za hivi karibni mwanadada Tunda aliweka wazi baadhi ya picha zikimuonyesha akiwa na mtangazaji wa Clouds Tv , Casto Dickson na kusemekana kuwa waili hao kwa sasa ni wapenzi na inavyosemekana ni kuwa mwanadada huyo kwa sasa ni mjamzito.
Mapya yameibuka baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kama Don Posh ambae alishawahi kuwa miss arusha na kusema kuwa anamuomba Tunda amuache Casto kwa sababu ni baba wa mtoto wake.
Chanzo cha habari kinasema kuwa mwanadada huyo na Casto walikuwa katika mahaba mazito kwa kipindi cha nyuma kabla hata ya kuwa na tunda na mpaka kufikia hatua ya casto kwenda ukweni na kujiambulisha ambapo baada ya hapo mwanadada huyo ilijulikana kuwa ana ujauzito wa Casto Dikson.
Kadri siku zilivokwenda mapenzi kati ya Casto na Posh yalizidi kunoga tena hasa baada ya dada huyo kujifungua watoto wawili mapacha mabapo hayo yalikuwa yakionekana kutokana na dada huyo kuwa anaweka picha za watoto wake na kumtag baba huyo aliyekuwa akijulikana kama baba wawili.
Kabla hata mwisho wa penzi la Casto , Posh na watoto wake halijajulikana mwafaka wake, zilianza kusambaa picha ambazo zilikuwa zikiwaonyesha Tunda na Casto wakiwa pamoja na huku zikionekana kuwa na mahaba fulani.
Baada ya gazeti la kampuni ya GPL, kusikia maneno hayo kutoka kwa wanyetishaji mbalimbali waliamua kumtafuta Posh mwenyewe ili kuhakikisha swala hilo ambapo alisistiza kuwa ni kwlei kwa waliyoyasikia na kuongezea.
Siku ya kwanza nakumbuka nilipoziona zile picha nilimuuliza Casto lakini alisema kuwa zile zilikuwa picha tu,na nikaamini kabisa kwa sababu najua kabisa mume wangu hawezi kummiliki mwanamke yule.siku nyingine tena nikaona picha wakiwa Club Next Door Masaki, nikashangaa sana, ila ninachotaka kutoka kwa Tunda aniachie baba wa watoto wangu, asimfanye kama king mswati sitaki.Atambue kuwa nimzaa nae mapacha ,yeye anajua wapi nimetoka nae?
Baada ya hapo Casto pia alitafutwa kujibu tuhuma hizo ambapo alifunguka kama hivi.
Kweli huyo tulishakuwa nae nakuzaa nae lakini tulikuja tukaaachana, sio yeye tu yupo muna na yupo mwanamke mwingine nilishazaa nae, lakini mbona wenzake hawasemi.ananiona niko na tunda ana-complain.kwanza huyo posh alikwa anataka kuolewa nikamwambia asubiri watoto wakifikishe mwaka ndio afanye mambo yake.