Dogo Janja Awatolea Povu Zito Wanaoiponda Ndoa Yake
Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja amewajia juu watu wote ambao bado wanaiponda ndoa yake na Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya.
Ndoa hii imezidi kutengeneza headlines kila kukicha pamoja na kwamba ilifungwa mwaka jana mwishoni na ndio ilikuwa stori ya kufungia mwaka lakini bado mpaka leo hii Ndoa hiyo imebaki kuwa gumzo.
Dogo Janja amedai kuwa amechoshwa na watu wote wanaomsema vibaya kuhusu ndoa yake na Kwenye mahojiano na Enews Dogo Janja amesema nyimbo yake ya Wayu Wayu ni ujumbe kwa wale watu wote wanaomsema vibaya kwa kufunga ndoa na Uwoya.
Walitokea watu walikuwa na kejeli na nini mimi naonekana kidagaa sina chapaa wananitukana nini lakini mwisho wa siku nawakanyaga kama soksi zangu ilikuwa kama sehemu ya kufikisha maudhui kwa watu waendelee kuheshimu mahusiano ya mtu wasiangalie utofauti wowote kwenye mahusiano kinachotakiwa sana ni upendo kama watu mnapendana mnaheshimiana hivi vitu vingine ni vitu vya kawaida”.
Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Dogo Janja alimtolea povu zito Rapa Young Tusso aliyemwambia ameidhalilisha Arusha kwa kuvaa kama mwanamke kwenye video yake ya Wayu Wayu, Dogo Janja amesema hamfahamu Young Tusso na itakuwa vizuri kama ataendelea kuwa shabiki wake.