Dogo Janja Hana Adabu, Kaoa Bila Kufuata Utaratibu:Mama Uwoya

Wakati Dogo Janja na Irene Uwoya wakiendelea kufurahia maisha yao ya ndoa, huku nyuma mama mzazi wa Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa hampendi hata kidogo  Dogo Janja kwa sababu hana adabu kabisa.mama irene alishawahi kulalamika na kusema kuwa hakuwahi kuwa na taarifa juu ya ndoa ya mtoto wake na Irene Uwoya kwa sababu alichokuwa  anajua ni kwamba mtoto wake alishaolewa na Ndikumana .

Siku chache zilizopita  Irene alisema kuwa anashindwa kuwakutanisha mama yake na mume wake kwa sababu mama yake amekuwa busy sana na safari nyingi ambazo zinamfanya kutokaa nyumbani kwa muda mrefu hivyo amekuwa akienda nyumban na kukutana na baba yake tu.

download latest music    

Akiongea na gazeti la mwananchi jumatatu hii, Mama Uwoya amesema kuwa hata kama kuja kujitambulisha asingewapokea kwa kuwa Dogo Janja hana adabu kabisa ndio maana amefunga ndoa bila kufuata utaratibu.

Mama yake na Uwoya amezungumzia swala la irene kusema kuwa yeye muda mwingi amekuwa akisafiri sio kweli kwa sababu hata kama anasafiri haiwezi kuwa mwaka mzima na amekuwa akimtetea Dogo Janja kwa  sababu anajua wazi kuwa wazazi wake hawamkubali Dogo Janja.

Yaan ndugu mwandishi sijui nisemaje , lakini mambo haya sipendi kabisa kuyaongelea kwennye media,kwa sababu haipendezi kubishana na mtoto uliyemzaa mwenyewe kwa sababu mwisho wa siku yule ni mtoto wetu pamoja na kwamba anafanya mambo ambayo hayatupendezi kabisa.lakini mkae mkielewa kwamba ndoa hiyo sisi hatuielewi wala hatutaitmbua kabisa.

Mama Uwoya ansema kuwa ndoa hiyo itabaki kutambuliwa na hao ndugu zake irene ambao aliwaita na kumfungisha ndoa wakati wazazi wake wapo Dar Es Salaam

siku ambayo ndoa imefungwa ndugu zake na wazazi wake tulikuwepo laikini tulishangaa kuona ndoa imefungwa na hata tulipokuwa tukimuuliza  amjibu yake yalikuwa ni kwamba alikuwa akicheza movie, hivyo tuliamua kuachana nae na kwa kuwa huwezi kumlazimisha mtu akwambie ukweli kwa kile anachokiamini yeye.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.