Ninapokuwa Karibu na Wema , Basi Mafaniko Yanakuwa Mengi-Diamond
Ikiwa bado drama za kwenye mitandao zikiendelea , Diamond Platinumz amefunguka na kukiri kuwa mara zote ambazo amekuwa karibu na wema sepetu amekuwa akifanikiwa sana kuliko kuwa na mwanamke yeyote.
Diamond ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika radio ya Times Fm na kusema kuwa pamoja na kwamba watu wengi wamekuwa wakizusha kuwa wao wamerudiani alakini hayo hayana ukweli wowote bali wameamua kuwa marafiki kwa sababu sasa hivi wanataka kufanya kazi.
Ninapokuwa karibu na wema sepetu basi mafanikio yangu yanakuwa mengi, hivyo wanaoona kuwa ukaribu wetu ni big ishu wanafeli sana na inakuwa sio poa sana .mimi na wema ni marafiki tu na hakuna uhusiano wa kimapenzi.
Hii inaweza kuthibitika kutokana na mafaniko makubwa aliyoyapata hivi karibuni msanii huyo baada ya kugombana na Zari na kuwa karibu na wema sepetu na mpaka kutoa album yake mpya, lakini swali linakuja kuwa mbona alipokaa na zari kwa zaidi ya miaka mitatu nyuma Diamond amefanya mambo mengi makubwa , je Zari hakuwa moja ya vitu vilivyomuongezea mafanikio.