Mke wa Roma Amshukuru Vannesa Mdee, ni Baada ya Mumewe Kufungiwa.

Mke wa msanii Ibrahim Mussa maarufu kama Roma amefunguka na kumshukuru Vannesa Mdee kwa kile alichokiongea siku ya kukutana na Naibu Waziri wa habari sanaa na michezo baada ya kuonyesha kumtetea msanii mwenzie Roma ambae amefungiwa kufanya kazi zake za sanaa kwa kile kinachodaiwa kutoa wimbo usiokuwa na maadili.

Mama Ivan kwa jina lingine Nancy ambae amejifungua hivi karibuni amemshukuru sana Vannesa na kusema kuwa anashangaa kuona kuwa ni msanii Roma pekee ndio amekuwa akiandamwa na mambo yote hayo na wala sio msanii mwingine yoyote.Nancy anasema kuwa kuna wakati mpaka amekuwa akitaka mwanaume wake aachane na kazi ya muziki kwa sababu anaona inamtesa.

download latest music    

Mungu akubariki sana wifi yangu, asante sana Vannesa Mdee, ila mume wangu anakutana na wakati mgumu na changamoto nyingi sana kwenye muziki wake , kuna muda mpaka natamani aache muziki kabisa lakini nakuwa najiuliza kwanini kila siku wewe tu,haina tatizo endelea kupambana kwani hata hili pia litapita.

Mwaka uliopita msanii roma alitekwa na watu wasiojulikana  na kupatikana baada ya siku tatu lakini mpaka sasa hakuwahi kufunguka kwa nini na wapi alitekwa, mwaka huu tena msanii huyo amefungiwa tena nyimbo zake na kutochezwa kituo chochote , mbaya zaid hata yeye amekatazwa kufanya kazi yoyote inayohusiana na muziki.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.