Mtangazaji Amuandikia Naibu Waziri Barua ya Wazi Kuhusu Wasanii na Muziki

Baada ya kufanya mahojiano na waandishi wa habari pamoja na wasanii na baadhi ya mashabiki wakiwepo ambapo Naibu Waziri wa sanaa alitoa nafas ya kuuliza maswala ambapo maswali yaliyoulizwa yalikuwa ni mengi lakini ilishindikana kupatikana kwa majibu mazuri ya kuwaridhisha wasanii pamoja na mashabiki wake , moja ya watangzaji wa Clouds Radio  Bamy baby wa kipindi cha XXL amemuandikia barua nzito na ndefu naibu waziri Mh Juliana Shonza kuhusu madai ya kuwafungia wasanii na kazi zao kwa ujumla.

Mamy Baby anaanza kwa kumwambia kuwa anatamani sana katika uongozi wake huo angeacha  alama kubwa na historia ya kuwasaidia vijana wenzake lakini pia kama mwanamke aache historia ya kukumbukwa akiwa kama mama na mlezi wa watoto.

download latest music    

Barua hiyo kwa naibu waziri inamtaka kuangalia ndoto walizonazo wasanii za kuwafikia wasanii wakubwa wa huko nje kwa kuwapita au kufanya nao kazi lakini kwa style aliyokuja nayo naibu waziri niwazi kuwa muziki wa bongo unaelekea kufa tena hili linakuja bila vipingamizi.

Mamy Baby amemfananisha Roma na Casper novest ambae amekuwa ni moja ya wasanii wakubwa nan waliofanikiwa na kusema kuwa endapo kutakuwa na sapoti ya kutosha kutoka serikalini basi inawezekana kabisa kuwa wasanii wa tanzania wanaweza kumfikia huyo na wengine wengi.

Mamy  Baby anasema kuwa siku zote alikuwa na ndoto kubwa ya kuwaona wasanii wa tanzania wakindesha magari ya kifahari, nyumba na maisha mazuri lakini kumbe hizo ni ndoto ambazo haizwezi kutimia kwa style ya nchi yetu.

Mtangazaji huyo anasema kuwa Naibu Waziri alitakiwa kujenga urafiki mzuri sana kati yake na wasanii wa ndani ili kukuza muziki huu ili siku moja wasanii wa tanzania waende nje kuimba katrika viwanja vikubwa na wala sio katika migahawa tu.

Haya yote yanakuja baada ya naibu waziri huyo kuwafungia wasanii wengi nchi kufanya kazi na baadhi ya nyimo kwa madai kuwa nyimbo hizo zimekuwa hazina maadili hata kidogo na zimekuwa zikipotosha jamii.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.