Aunty Ezekiel Amkana Zari Mchana kweupe
Baada ya familia ya Diamond na marafiki wa Diamond kuamua kuamisha majeshi yake kwa Wema Sepetu pia hivi karibuni msanii wa kike wa bongo movie Aunty Ezekiel amekuwa akionekanakuwa karibu na wema sepetu na hivyo watu kuanza kumuona kama msaliti kwa sababu kipindi diamond yupo na zari pia msanii huyo alikuwa akionekana kuwa karibu na zari hata kufikia hatua ya kuwa anakwenda na kuonekana wote wakiwa Afrika ya Kusini
Baada ya kuulizwa na waandishi wa habari juu ya watu kumuita msaliti, Aunty Ezekeiel alisema kuwa
Sipendi sana watu wanavyokuwa wananiongelea juu ya swala hilo la ikariu wangu na wema,waniache kabisa kwani sikuwa rafiki wa zari na siwezi kumsema vibaya , wema atabaki kuwa rafiki yangu siku zote , maneno ya watu hayawezi kuniweka mbali na wema.huu ni uamuzi wangu kwa sabau nilikuwa karibu na Zari na hayo ni maamuzi yao mimi hayanihusu.
Hivi karibuni uhusiano wa Wema Sepetu na Aunty umeonekana kuwa umeiva sana hasa baada ya kuwa wote katika party ya Vikings Night ambapo walianza kuweka picha nyingi sana katika mitandao ya kijamii ndipo mashabiki walipoanza kumtolea povu na kumwambia kuwa kipindi Diamond alipokuwa kwa zari na yeye pia alikuwa karibu na Zari na sasa wamehamia wote kwa Wema.