Dogo Janja Awaombe Msamaha Mashabiki Zake Arusha -Young Tusso
Rapa anayefanya vizuri Bongo Young Tusso amedai Dogo Janja lazima akawaombe msamaha watu wake wa Arusha kwa sababu amewakosena sana kwa video yake ya wimbo wa ‘Wayuwayu’.
Dogo Janja alizua gumzo wikiendi iliyopita baada ya kuachia video yake ya wimbo wa Wayuwayu ambayo ilileta utata mkubwa sana kwani kwenye video hiyo ana one kama kuvaa kama mwanamke kuvaa kigodoro, kapaka make up na kuvaa wigi.
Kama unavyojua Dogo Janja anatokea Arusha Ngarenaro hivyo baada ya video hiyo kutoka watu wa Arusha walidai wamekasirika sana na kusema amewadhalilisha machalii wote wa Arusha.
Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Young Tusso amedai anaungana na Wana wa Arusha na kumtaka Dogo Janja akaombe msamaha kwani hakutakiwa kufanya vile kwani yeye ni mwana hip hop alafu ni mume wa mtu na mtoto wa Kiislamu.
Kwa msanii kama Dogo Janja kitendo alichifanya hakupata sawa nimeona msanii wa Hip hop alafu anafanya hivi? huyu jamaa anatoka Arusha tunatarajia Arusha itoe wagumu maana wanasemega Hip hop inatoka Arusha sasa inakuaje anafanya hivyo alafu isitoshe yule mume wa mtu na pia ni mtoto wa kiislamu kwa kweli nimeshangazwa kumuona Dogo Janja kawa bibie”.
Young Tusso amesisitiza kuwa amem-diss Dogo Janja kwa sababu hajakubaliana na yeye kuvaa kama mwanamke kwa sababu anaidhaliliishia hip hop lakini pia anakudhalilisha Arusha hivyo amemtaka akawaombe msamaha mashabiki zake wa Arusha.