Ndoa Ya Meninah Yadaiwa Kuwa Matatani

Mwanamuziki wa Bongo fleva Menina Abdulkareem maarufu kama Meninah amerudi tena  kwenye headlines huku ndoa yake ikiwa chanzo ambapo inadaiwa kuwa kuna matatizo yanayotaka kuvunja ndoa yake.

Meninah amefunga ndoa mbili kwa siri ambapo mwaka jana alifunga ndoa na mumewe wa sasa miezi michache baada ya kuachana na kupewa talaka na mume wake mwingine.

download latest music    

Lakini hivi sasa XXL ya Clouds Fm wanaripoti kuwa Ndoa ya menina na mumewe huyo ambaye amezaa naye mtoto mmoja iko matatani  na vikao vya familia vimefanywa ili kuwasuluhisha ambapo inasemekana kuwa Meninah anamjeuria mumewe.

Ambapo inasemekana kuwa wawili hao walikuwa kwenye ugomvi mzito hadi kufikia hatua ya Menina kumshikia kisu mumewe hadi kupelekea kumjeruhi vibaya mumewe na kwa habari za chini chini ni kuwa mumewe kaka wa hospitali sahivi.

Lakini pia Shilawadu wanaripoti kuwa kutokana na kitendo hiko alichokifanya Meninah kuna ubuyu unasema muda wowote anaweza kuonja segerea lakini alipotafutwa kuulizwa kuhusu ishu hiyo hakupokea simu na mumewe alikataa kuongea na kusisitiza ni mambo ya kifamilia.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.