Haitham Kim: Sina Tatizo na Master J Wala Marco Chali
Mwanamuziki wa Bongo fleva, Haitham Kim aliyetamba na vibao vyake kama ‘Playboy’ aliomshirikisha Wema Sepetu na ‘fulanI’’ amefunguka na kusema kuwa hana tatizo na Marco Chali wala Master Jay.
Haitham Kim alikuwa msanii aliyesimamiwa na label ya MJ Records ambapo kupitia wao alitoa ngoma hizo mbili lakini mwaka jana yeye pamoja na msanii Nini walimwagwa na label hiyo na producer aliyekuwa anawasimamia Daxo Chali kwa utovu wa nidhamu.
Lakini kulitokea bonge la varangati kwani Haitham aliibuka na kudai kuwa sababu pekee iliyomfanya Daxo Chali amtimue ni baada ya kumtaka kimapenzi lakini alivyomkataa na kusikia anatoka na Idris alimtimua hivyo hivyo kwa Nini alimtaka kimapenzi alivyokataliwa akawatimua.
Tangu wameondoka Mj records, Haitham Kim amekuwa akijisimamia mwenyewe na kazi zake lakini amekiri kuwa maisha yalikuwa mepesi zaidi alipokuwa chini ya label hiyo.
Kwenye mahojiano na Clouds Tv, Haitham amekiri kuwa hana tatizo na maproducer wengine katika label hiyo kama Marco Chali na Master Jay:
Kwanza nataka niweke wazi kuwa mimi sikuzinguana na Master Jay wala Marco Chali kama inavyozungumziwa Mj Records kama yenyewe mimi nilitofautiana na Daxo Chali ambaye ndio alikuwa anatusimamia kwaiyo kama itatokea nafasi nakarudi Tena Mj Records basi nitarudi kwa mkataba mwingine tofauti sio ule niliokuwa nafanya na Daxo kwasababu nimekaa pale label kwa miaka mitano nimeachia ngoma tatu tu wakati nimerekodi albamu tatu lakini mpaka leo hawajanipa ngoma zangu na mpaka wakafuta video yangu ya playboy kwenye YouTube”.