Jokate Ahaidi Kuwashika Mkono Wanawake
Mfanyabiashara na mmiliki wa brand ya Kidoti, Jokate Mwegelo amewatolea ofa wanawake wajasiriamali wote ya kuwashika mkono kwenye biashara zao kwa kusaidia kuwatangazia biashara.
Jokate alianza kupata umaarufu baada ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006/ 2007 na kuwa mshindi wa pili tangia hapo Kidoti aliendelea na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam mpaka alivyomaliza masomo yake.
Jokate alijiingiza kwenye biashara na kutengeneza kampuni yake ya Kidoti ambayo imemletea mafanikio mengi sana na kukua kwa kasi ya ajabu mbali ya kuwa mfanyabiashara Jokate pia hivi sasa ni mwanasiasa wa CCM na ni kaimu Katibu wa uhamasishaji UVCCM.
Jokate baada ya kupata mafanikio hayo amefunguka kuhusu nia yake ya dhati kabisa ya kutaka kusaidia vijana hasa Wanawake ambapo kwenye ukurasa wake wa Instagram ametangaza fursa ya kuwatangazia Wanawake biashara zao:
Wanasema kutoa ni moyo na sio utajiri kuna wengi wana vingi lakini mioyo yao migumu kutoa na wapo ambao wako tayari kugawana kile chao cha mwisho hata ikimaanisha wasibaki na chochote ilimradi wewe upate na ufanikishe lako. Mpaka kufika nilipofika Mwenyezi Mungu amenipa watu wengi sana wakunishika mkono na kunisogeza karibu na ndoto yangu. Nimepitia kurasa zenu na kusoma matamanio yenu. Naomba mwaka huu kwa ajili ya sikukuu ya Wanawake Duniani naomba nifanye kitu tofauti kidogo naomba Wanawake/ wadada chini ya miaka 35 wake kwangu na biashara wanazofanya na mimi nitawa support tutawapa kiasi cha shilingi milioni 1”.