Baraza Kutoa list Nyingine ya Wasanii na Nyimbo Zisizokuwa na Maadili
Ikiwa bado wasanii mbalimbali wakiendelea kulalamika na kusema kuwa baraza la sanaa limekuwa likiwafungia bila kutoa sababu za kufungiwa kwa nyimbo nyingi za wasanii, baraza la sanaa linajiandaa kutoa nyimbo nyingine ambazo zitachunguzwa na zikaonekana kuwa na tatizo la kuwa zimeenda kinyume na maadili ya Tanzania.
Wiki iliyopita baraza la sanaa lilitoa list ya nyimbozaidi ya 10 ambazo zilitakiwa kufungiwa kuchezwa katika vituo mbalimbali vya habari kwa madai kuwa zimekiuka vigezo na masharti na maadili ya tanzania huku msaii wa hip-hop roma mkatoliki akifungiwa miezi sita kutokujihusisha na kazi za sanaa zozote kwa muda wote huo kutokana na kuwepo kwa baadhi ya maneno yenye matusi katika wimbo wake wa kiba100 aliomshirikisha Stamina na Maua Sama.
Hata hivyo baraza la sanaa linaendelea kuchunguza nyimbo nyingine zilizopo katika muziki na hata zinazoendelea kutoka ili kujiridhisha na maadili yanayopatikana katika nyimbo hizo na kama kutakuwa na ukiukwaji wa taratibu pia baraza haliwezi kusita kufungia nyimbo hizo au wasanii.
Baraza linawataka wasanii wote kupeleka nyimbo zao katika mamlaka husika kablya ya nyimbo hizo kutolewa na kusambazwa kwa mashabiki ili kuondoa usumbufu unaojitokeza sasa hivi wa kufungiwa.
Huu ni muendelezo na utekelezaji alioanzishwa Mh Naibu Waziri wa habari, tamaduni sanaa na michezo alipoanza kwa kuwafungia wasanii wa kike ambao wamekuwa wakiweka picha za uchi katika mitandao hivyo zoezi ili litakuwa ni kwa ajili ya wae tu wanaokiuka taratibu na kuvunja maadili ya watu katika jamii.