“Natamani Ningekuwa na Mabwana Sita Ili Mmoja Aninunulie Simu Maisha Yangu Yaendelee”- Faiza Ally
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu kwenye mitandao ya kijamii Faiza Ally amefunguka kuhusu kipindi kigumu anachopitia baada ya simu ya yenye thamani ya milioni tatu kushikiliwa na polisi kwa zaidi ya miezi mitatu.
Miezi michache iliyopita Faiza aliacha umma wa Watanzania midomo wazi baada ya kuamua kuanika picha yake mtandaoni akiwa uchi wa mnyama Leba wakati anajifungua mtoto wake wa kiume.
Baada ya kusambaa kwa picha hiyo Faiza alitakiwa kuwasili kituo cha polisi mara moja kwani iliangaliwa kama ni picha ya uchi na ni kinyume na maadili ya Kitanzania na alipofika kituoni hapo simu yake ilichukuliwa kama ushahidi.
Faiza leo kaamkia Instagram kulalamika juu ya suala hilo na ameandika maneno yafuatayo:
Kama kuna siku nimeamka na maumivu makali ni leo, leo nimetamani ningekuwa mzungu niishi kwenye nchi zenye haki za binadamu maana kuna wakati unaonewa kwenye nchi yako! Huu ni mwezi wa tatu tangu polisi wachukue simu yangu iphone 7+ yenye thamani ya shilingi milioni 3 inaniuma sana naenda kuripoti polisi sahivi nimepewa wiki mbili mbili kisa picha yangu ya leba wanahesabu kama pornography, Nimewaeleza polisi changamoto ninazopitia kwa kukosa simu mimi ni mfanyabiashara shughuli zangu zote zinategemea ile simu kuna emails contacts hata picha za biashara maisha yangu bila hiyo simu ni magumu mimi ni kama wa watoto wawili mimi ndio nilipe ada ya mwanangu, kodi ya nyumba na maduka, ugali wa watoto ninunue”.
Lakini pia Faiza ametamani angekuwa na mabwana hata sita wamsaidie kununua simu mpya:
Nimewaza mpaka nimetamani ningekuwa na mabwana kama Sita hivi ili mmoja aninunulie simu niendelee na maisha yangu najitahidi nisimame bila mabwana lakini wakati mwingine wanawake tukizidiwa hakuna namna sasa hivi sio sawa mnakuwa kama mnarudisha juhudi zangu nyuma naomba mtoe huku ili maisha yaendelee”.