Wema Atangaza Kuajiriwa na Diamond Ndani ya Wasafi.
Ikiwa bado muafaka wa penzi lake(diamond ) na mama wa watoto wake Zari the Bossy bado haujafahamika kwa sababu amekuwa kimya wa muda mrefu, siku ya tarehe 4 March Wema amefunguka mazito juu ya uhusiano wake na Diamond ambae alikuwa mpenzi wake kwa miaka kadhaa nyuma na kuweza kugombana kwa kurushiana maneno katika mitandao.
Akihojiwa na vyombo vya habari Wema Sepetu amesema kuwa wao ni marafiki wakubwa na wanakoelekea ni kuwa mtu na bosi wake kutokana na kwamba mwanadada huyo anategemea kuwa na kipindi katika studio mpya za Wcb.
Mimi na Diamond we are just gud friend na hivi karibuni anaenda kuwa bosi wangu kwa sababu ninaenda kuwa na kipindi cha kukiendesha ndani ya Wasafi.-Alifunguka Wema.
Wema ambae siku za nyuma alikuwa akituhumiwa na Zari The Bossy kuwa ndio sababu kubwa ya mwanamama huyo kuachana na mwanaume wake , anaonekana kutokuwa na uoga wowote wa kuwa karibu na Dimaond na hata kufanya kazi pamoja kitu ambacho watu wengi hawakukitegemea kutoka kwa wawili hao.
Ingawa kwa upande wa Diamond imekuwa ni vigumu kwa watu kuamini kuwa kama angeweza kukaaa kimya kwa muda wote huo tangu mzazi mwenzie alipotangaza swala la kuachana nae rasmi.
Akijitetea kuhusu uhusiano wake na Wema sepetu , Diamond siku zote amekuwa akisema kuwa watabaki kuwa marafiki na kufanya kazi pamoja hata kama mwanzo walikuwa maadui.Na kwa upande wake amekuwa akisema kuwa uadui wao umekuwa ukisababishwa na mashabiki zao na utoto waliokuwa nao kipindi.