Diamond na WCB Wamuegemea RC Makonda

Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa label maarufu ya WCB, Diamond Platnumz na timu yake nzima imefunguka na kusema inamtegemea Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kusimamia suala la nyimbo kufungwa.

Siku chache zilizopita Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza rasmi kuwa jumla ya nyimbo 13 za wasanii mbali mbali zimefungiwa akiwemo Diamond ambaye alifungiwa nyimbo zake mbili ambazo ni Halelujah na Waka waka.

download latest music    

Tangu taarifa zisambae kuwa nyimbo mbili za Diamond zimefungiwa Kumekuwa na hisia hasi juu ya suala hilo na sio ndani tu ya Tanzania bali hata kwa mashabiki walio nje ya Tanzania.

Lakini tangu sakata hilo litokee Diamond hajaongelea chochote kuhusiana na ishu hii lakini uongozi wake meneja wake Salaam Sk amefunguka na kusema hawawezi kuongelea suala hilo ila kama kuna mtu ana maswali juu ya hilo akaongee na malezi wao RC Makonda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Salaam SK aliandika ujumbe huu juu ya ishu hiyo:

Habari za muda huu waungwana, Tumepigiwa simu na waandishi wa habari kila kona kuhusu nyimbo mbili za Diamond zilizofungiwa, nimeona kama taasisi huwaga tunafanya vitu kwa kutokukurupuka sie kama WCB tulipoona taasisi yetu inakuwa kubwa tukaomba ulezi kwa Paul Makonda ambaye ni kiongozi wa serikali mwenye kupenda maendeleo ya vijana kwaiyo nyimbo zote za WCB kabla ya kutoka lazima azipitie, kuna nyimbo nyingi ameshazizuia na zinazotoka ameziridhia yeye binafsi zitoke, kwaiyo sioni sababu ya nyimbo ya halelujah na wakawaka kufungiwa kama inavyosemekana  maana sisi hatujapata barua ya nyimbo hizo kufungiwa na kama zimefungiwa mlezi wetu ataongea zaidi”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.