Eric Omondi Aomba Radhi Baada ya Video Yake Ya Utupu Kusambaa Mtandaoni
Mchekeshaji maarufu kutoka Kenya Eric Omondi ameomba radhi baada ya video yake ya utupu kusambaa mtandaoni na kusababisha kuzuka kwa sintofahamu.
Video hiyo ya Eric ilimuonyesha akiwa uchi wa Mnyama akiogelea mtoni/ziwani akiwa na watoto wa kiume wengi sana ambapo makalio yake yalikuwa wazi huku akiwaonyesha watoto utupu wake.
Kilichoibua hisia za watu wengi ni suala la yeye kuonekana akiwa uchi wa mnyama na watoto wa kiume wadogo ambao wanaweza kuwa na umri kuanzia miaka 7-14 na wenyewe wakiwa uchi wakiwa wanaogelea.
Baada ya video ile kuingia mtandaoni kila mmoja alikuwa na lake la kusema kuhusu video hiyo huku kuna baadhi ya watu wamefikia hatua ya kumrushia maneno ya kejeli na hata kumuita shoga kwa kuogelea uchi na watoto wadogo wa kiume.
Erick Amejitokeza na ameomba radhi kwa video hiyo huku akisisitiza kuwa ilikuwa kama utani kwani na yeye ni mchekeshaji hakuwa na lengo la kumkwaza mtu yoyote.