Snura hajashangazwa Kuona Ngoma ya Chura kufungiwa.
Malkia wa ngoma za uswazi Tanzania Snura Mushi maarufu kama Snura Majanga amefunguka na kusema kuwa hajashangazwa hata kidogo kuona ngoma ya chura imegungiwa lakini anachoshangaa ni kwanini wimbo wake wa nimevurugwa nao pia kufungiwa wakati ni wimbo wa siku nyingi.
Snura anayaongea hayo baada ya jana tarehe 28 February kutoka list ya nyimbo zaidi ya kumi kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania BASATA kwa madai kuwa nyimbo hizo zimekosa maadili ya kusikilizwa na kuonekana katika vituo vya habari nchini.
Kufungiwa kwa nyimbo hizi ni muendelezo wa kazi ya BASATA likiwa na nia ya kufungia na kukataza nyimbo zote na wasanii wote ambao wamekuwa wakitoa nyimbo au kuchapisha picha ambazo hazina maadili.
Snura anasema kuwa wimbo wa nimevurugwa ni wa zamani sana ukilinganisha na nyimbo yake ya chura na hata za wengine zilizofungiwa kwa sababu ni za hivi karibuni, hata hivyo nbado Snura anasema kuwa hajapata taarifa rasmi kutoka BASATA kuhusu kufungiwa kwa nyimbo zake zaidi ya kuona taarifa hizo katika mitandao tu.
Wasanii wengine walofungiwa ni pamoja na Diamond, Ney wa mitego Gigy money , Barnaba.