Waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania Wajivua Rasmi Katika Mashindano Hayo
Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency ltd, iliyokuwa ikijihusisha na kuandaa mashindano ya miss tanzania nchini hashim lundenga ametanga kujivua rasmi katika uandaaji wa mashindano hayo na hatohusika katika kuyaandaa tena tangu february 13 mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari nchi, Hashim Lundenga amesema kuwa lengo kubwa la wao kuachana na maandalizi ya mashindano hayo ni kwa sababu anataka damu changa iingie katika uandaaji wa mashindano hayo ili kuleta changamoto na mabadiliko katika mashindano hayo.Hata hivyo mashindano hayo yamekabithiwa kwa kampuni nyingine inayojulikana kama The Look ikiongozwa na mrembo Basila Mwanukuzi ambae aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998.
Tumefikia hatua hii baada ya kuona kuwa kampuni yetu tayari imeshajipatia sifa nchini,hivyo tunaamini kuwa The Look Company Limited chini ya mkurugenzi wake Basila Mwanaukuzi watasimamia kanuni,taratibu, sheria na miiko ya uongozi na hatimaye kumpeleka mrembo katika mashindano ya dunia kama ilivyo kawaida.
Kwa kuongezea, mkurugenzi mpya wa mashindano hayo chini ya The Look Company Basila Mwanaukuzi amesma kuwa wamejiandaa vya kutosha kufankisha mashindano hayo na kuendeleza mazuri ya pale Lino Agency Ltd walipoishia.na kusema kuwa pale wanapoona kuwa na changamoto hawatasita kuwa karibu na LINO na BASATA ili kufanikisha kila linalowezekana.
Hashimu Lundenga amewashukuru sana Baraza la Sanaa Tanzania kwa kipindi chote walichokuwa wakifanya kazi pamoja ukiachana na changamoto nyingi walizopitia, na kuomba kuwapa ushirikiano waandaaji wapya.
Mashindano ya Miss Tanzania yalikuwa katika hali isiyokuwaya kueleweka hata kusababisha kukosekana kwa mashindano hayo mwaka uliopita kutokana na kukosekana kwa udhamini uliosababishwa na uongozi mbaya.