Jike Shupa Apata Tetesi za Kufuga Mateja Nyumbani Kwake.
Mwanadada anayeuza sura katika video za wasanii mbalimbali almaarufu kama JikeShupa amekumbwa na tetesi za kufuga watumiaji wa madawa ya kulevya nyumbani kwake na kwamba mateja hao wamekuwa na athari kubwa katika mtaa huo.
Hivi karibuni mwanadada huyo alifunguka na kukubali kuwa alikuwa akikaa na mdogo wake na mbunge wa chadema Esther Bulaya ambae mdogo wake ameathirika na matumizi ya madawa ya kulevya ambae alikuwa akihitaji mtu wa karibu wa kukaa nae kwa kipindi hiki ambacho alikuwa akipatiwa matibabu.
Jike shupa ambae anakaa maeneo ya Mwananyamala hospitali inasemekana kuwa amekuwa akikaa na watumiaji wa madawa ya kulevya zaidi ya mmoja na kwamba amekuwa akiishi nao kinyume cha utaratibu kitu kinachowatia wasiwasi hata majirani zake.
Jike shupa anawafuga mateja kwakweli kwa sababu anachumba maarumu kabisa ambacho wanakaa,na wengi wao ni wale wanaotumia madawa kwa ajili ya kuacha unga.watu wanadai kuwa kuna kitu atakuwa anafaidi kwa sababu anakaa nao na kuna muda watu wanalaamika kuwa wanapora alafu wanamletea yeye mama yao.-Aliongea mmoja wa wakazi wa mtaa anaokaa jike shupa
Alipotafutwa jike shupa kujibu tuhuma hizo alikubali kuwa ni kweli amekuwa akikaa na watu hao kwa muda mrefu kwa sababu walikuwa wakituma dawa za kuacha madawa ya kulevya lakini sasa hivi walisharudi makwao na wala hawapori watu.
sio kweli kwamba walikuwa wanapora watu mitaani,lakini walishamaliza dawa za kufanya waache kutumia unga na sasa waisharudi makwao.-Alifunguka jike shupa.
Hpo awali jike shupa alishawahi kukumbwa na tetesi za kuwa anawafuga mashoga nyumbani kwake na kufikia hatua ya kugombana na majirani zake.