Dayna :Sifikirii Kutoa Album Sasa Hivi kwa Sababu Wengine Wametoa
Mwanadada ambae hivi juzi amekuja na wimbo mpya huku mitaa mbalimbali katika mitandao wakimzushia kuwa yeye ni mama kijacho amefunguka na kuelezea kuwa hata kama kuna watu wengi kwa sasa wamekuwa wakitoa album lakini kwa upande wake hajafikiria kufanya album kwa sasa hivi kwa sababu anaona kwamba bado hajaitaji kutoa album ya muziki wake.
Dayna Nyange anasema kuwa mashabiki wengi wanakuwa wanawashinikiza sana wasanii kuiga wasanii wenine kufanya kile walichofanya wenzao kwa sababu tu fulani kafanya , bila kujua kuwa kila kitu kina kuwa na wakati wake katika kazi.
sijafikiria kutoa album kwa sasa hivi kwa sababu wenzangu wametoa album,mimi ni mtu ambae ninafanya kitu kwa muda wangu sahihi na muafaka na sio kufuata mkumbo kwa sababu tu fulani amefanya kitu hicho.siwezi kufanya ili nionekane kuwa tu nina album hapana, bali nahitaji kufanya album ambayo itakubalika.Alisema Dayna Nyange.
Hivi karibuni wasanii wa tanzania wameanza kuachia album zao akiwepo msanii pekee wa kike Vannesa Mdee ambae hata bada ya kuachia album yake ya money monday alikuja na kutoa mrejesho kuwa mashabiki wake wameipokea album hiyo vizuri na mauzo yanakwenda vizuri.