Sugu Ahukumiwa Jela Miezi Mitano.
Mwanamuziki mkonge nchini Tanzania ambae pia baadae aliamua kujiingiza kwenye siasa na kuendelea na kazi zake za muziki akiwa mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi almaarufu kama Mr. Sugu amehukumiwa miaezi mitano jela baaada ya kukutwa na hatia ya kumkashifu Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hukumu hiyo ilitolewa jana February 26 katika Mahakama ya mkazi jijini Mbeya , ambapo Mh. Sugu pamoja na mwenzake walihukumiwa kifungo hicho na kuanza kukitumikia mara tu baada ya kupokelewa kwa hukumu hiyo.
Mr. Sugu alikuwa ni moja ya wasanii wakongwe wa zamani waliipeleka sanaa ya muziki wa Tanzania mbali na kupigania sana haki za wasanii mara baada ya kujiingiza katika siasa na kuongelea sana matatizo ya wasanii akiwepo Bungeni.
mh .Sugu alipokuwa mahakamani jana na watu wake wa karibu.