Alikiba na Abdulkiba Kufunga Ndoa Siku Moja
wasanii wa kizazi kipya nchini ambao ni ndugu Abdul Kiba na kaka yake Ali Kiba ambao wanaunda kundi la Kiba Square inasemekana kuwa wanatarajia kufunga ndoa kwa pamoja hivi karibuni.Watu wa karibuni wa familia hiyo wanasema kuwa wasanii hao tayari wameshaanza kufanya vikao vya harusi huko nyumbani.
Hivi ninavyokwambia ni kwamba vikao vya hausi tayari vilishaanza kimya kimy lakini vinahusisha ndugu wa karibu tu wa familia basi.
Itakuwa ni harusi kubwa kwa sababu ni ya watu wawili mabao ni maarufu sana bongo na nje ya bongo na wamependa kuifanya harusi hiyo kimya kimya kwanza.na kwa sababu kila mmoja anamashabiki wengi kwaio itakuwa na watu wengi sana.
Mnyetishaji wa habari hizo anasema kuwa hata ile nyumba ambayo Alikiba ameijenga alipewa agizo na mama yake kuijenga lakini aliambiwa kuwa hapaswi kuamia katika nyumba hiyo mpaka pale atakapo oa ndio aweze kuhamia na mke wake.
Hiyo nyumba ya Tabata inamsubiri tu Kiba amalize kuoa kwanza ndo ahamie kwa sababu ina kila kitu ndani kikubwa kilichokuwa kikisubiriwa ni harusi tu.
Baada ya kampuni ya habari ya GPL kupata habari hizo kutoka kwa watu wa karibu waliamua kumtafuta Abdul Kiba ili kuweza kuthibitisha habari hizo ambapo mwandishi alianza kwa kumuuliza kwanini amekuwa kimya au mipango ya harusi ndio inamfanya anakuwa busy ndipo Abdul Kiba alipojibu
Harusi ya Ali au?,anayeoa ni Ali mimi sina mpango wa kuoa mwaka huu kabisa.Si unajua mambo ya wanawake, ndoa mimi bado Ali ndio anategemea kuvuta jiko mwezi uja.
Hata hivyo tetesi zilizopo ni kwamba Ali Kiba anatarajia kumuoa mwanamke kutoka mombasa.