Idris aongelea uchungu wa mama kupoteza ujauzito mwaka moja baada ya Wema Sepetu kupoteza mapacha wao

Wema Sepetu na Idris Sultan walikua wanatajaria kupata watoto mapacha lakini ujauzito wa Wema ulipotea ghafla Februari 2016.

Wema alidhibitisha kupotea kwa ujauzito wake kupitia Instagram ambapo alieleza uchungu wa kuwapoteza wanawe wawili. Idris pia alieleza uchungu aliyokuwa nayo kwa kwa Instagram.

download latest music    

Mwaka moja baada ya tukio hilo, Idris ameandika kuhusu dhiki inayowakumba kinamama wanapopoteza ujauzito wao.

Idris aliandika ujumbe huo siku moja baada ya ulimwengu nzima kusherekea siku ya mama duniani. Soma alichoandikwa Idris hapo chini:

“Dear Mama,

Naomba nianze na kuomba samahani kwa niaba ya wote waliokusahau, tumejisahau sana na tupo chini ya miguu yako. Kuna anayesoma akidhani namuongelea mama yangu mzazi ila sio. Namuongelea mama ya dunia, mama aliyeizalia dunia, mama anayepigana kupata mtoto bila mafanikio, mama aliyepoteza watoto, mama aliyeharibika mimba, mama anayeangalia wenzake wakipata watoto kila kukicha anaalikwa kwenye arobaini za wenzake na anajipa moyo na matumaini ipo siku atawaalika kwenye yake. Tumepewa nguvu na uwezo wa kupendana pale tunapoona mapungufu tunapeana moyo. Sina dhumuni la kumkashifu yoyote aliyetoa mimba kwani watoto ni mipango tofauti kwa kila mama. Naomba niweke mwanga kwa yule mama aliyepoteza watoto aliowapangia hadi shule gani watasoma, akanunua hadi kitanda cha mtoto akapamba na chumba kabisa. I need you to know your baby(babies) love you. Mnaweza mkawa hamjapata nafasi ya kuonana ila kwa ule mda mfupi walioishi ndani yako ni the happiest time of their life. Usithubutu hata siku moja kukaa na kufikiria labda ungefanya tofauti isingekua ilivyotokea nooooo you did all you could na Mungu atakupa mengi zaidi. Mama sio lazima uwe na mtoto ila kila unayemfunza kitu, unayemshauri, uliyemsaidia akapata hata chakula wewe ni mama kwake. Jana unaweza ukawa ulilia sana ila leo naomba nikukumbushe kuwa we have your back anytime anyday with un-ending love. Happy mothers day kwako mama ☺️??

With love,

Baba aliyepoteza watoto.”

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere