Lulu Diva:Siogopi Kitu Nikitaka Kuachia Ngoma Mpya
Mwandada anaefanya vizuri sasa hivi na ngoma yake mpya ya amezoea , Lulu Abbas marufu kama Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amekuwa na ujasiri wa kuthubutu na kutokuogopa kitu chochote kila anapotaka kuachia ngoma yake mpya hata kama wapo watu watakaokaa wakamponda kuhusu nyimbo zake.
Akiongea na Dizzimonline, Lulu Diva ansema kuwa anaamini kuwa kama muziki ni mzuri siku zote ni lazima utaonekana tu hata kama wapo watu watakaa na kuanza kuongelea vibaya muziki huo.Diva anasema kwa kwa sasa ameshajifunza kufanya vitu bila kuogopa ni kitu gani kinachukua nafasi katika mitandao kwa kipindi hicho, hivyo kama anaamua kutoa nyimbo yake hana kinachomzuia.
Mimi siogopi kitu kama nataka kuachia ngoma yangu hata kuwe kunaendelea nini katika mitandao ya kijamii kwa muda huo wa sababu mimi ninaamini kuwa kama muziki wako ni mzuri hakuna kitakachokufanya usionekane so nikuweka jitihada tu katika kazi na maandilizi ni sumu peke yake.
Lulu Diva anasema kuwa kwa mwaka huu ameamua kuwakonga mashabiki zake kwa sababu amejipanga sana na anaayarajia kudondosha ngoma nyingi.
Kumekuwa na tabia ya wasanii wengi kuwa wanasubiria kama kuna kitu kikubwa kina-trend katika mitandao wakiogopa kuwa trending iyo inaweza kufanya muziki wao kufunikwa.