Dj Sinyorita Aelezea Maisha ya U-Dj na Urembo

Anaweza kuwa ndie dj wa kwanza Tanzania kwa sifa za kuwa dj bora wa kike , lakini pia amekuwa ni dj anaefanya kazi yake vizuri sambamba na urembo na ubora wa unadhifu wa muonekano wake.Anajulikana kama Dj Sinyorita moja kati ya dj bora wa kike.

Akiwa katika kazi yake siku zote uonekana mrembo na muonekano wake sio kama ilivyozoeleka kwa ma-dj wengi wa kike ambao ujiweka kiume na kuvaa vibaya vibaya.Sinyorita siku zote amekuwa ni mtu wa kujiweka safi na kuonekana mrembo hata kuwafanya baadhi ya wanaume kumtolea mate.

download latest music    

Akielezea changamoto au umuhimu wa urembo katikakazi yake ambayo inamfanya awe tofauti na wenzake Dj Sinyorita ansema kuwa kwake urembo ni swala la kawaida lakini ni la muhimu kwa sababu kaiz yoyote mwanamke anapoifanya urembo uweza kumuongezea umaridadi katika kazi na hata anapokuwa kazini sio vizuri kuonekana kuwa yupo katika hali ya uchafu kwa sababu haileti picha nzuri anapokutana na watu wengi.

Dj na Urembo no sehemu ya maisha yangu, siwezi kuwa dj bila kuwa mrembo hata mara moja,kwa sababu siwezi kukaa sehemu nina mix alafu nikawa naonekana mchafu.ni lazima niwe mrembi ili nipate kuvutiwa, urembo ni kama vionjo niviweka katika kazi yangu ni kama vile ukitaka kupika pilau katika pilau lazima kuwe na vitunguu swaumu na nini na nini.lazima niwe smart na hata wasanii pia lazima wawe smart katika kazi si unaona kama kina Nandy, Lulu Diva wako smart.

akiongelea kuhusu dj ambae amekuwa akim-inspire kwa muda tangu amekuwa dj, Dj Sinyorita nasema kuwa ni wengi amekuwa akiwaangalia na kuwapenda na kupenda kazi zao kwa nje na ndani ya Tanzania.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.